Surat Al-Ahqaf, aya 35

46:35

فَٱصۡبِرۡ كَمَا صَبَرَ أُوْلُواْ ٱلۡعَزۡمِ مِنَ ٱلرُّسُلِ وَلَا تَسۡتَعۡجِل لَّهُمۡۚ كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَ مَا يُوعَدُونَ لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا سَاعَةٗ مِّن نَّهَارِۭۚ بَلَٰغٞۚ فَهَلۡ يُهۡلَكُ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ ٣٥

Fasbir kamā sabara ulul-'azmi minar-rusuli walā tasta'jil lahum ka annahum yawma yarawna mā yū'adūna lam yalbathū illā sā'atam min nahāri balāghun fahal yuhlaku illal-qawmul-fāsiqūn

Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayo yaona waliyo ahidiwa itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipo kuwa walio waovu tu? 35

Maelezo ya chini

35 Ewe Muhammad! Wastahamilie makafiri kama walivyo stahamili Mitume wengine wenye nguvu na imara wakati wa shida. Wala usiwahimizie adhabu. Kwani hiyo itawafika tu, hapana hivi wala hivi, hata ikichukua muda mrefu. Siku watapo kiona kitisho chake watadhani kuwa hawakukaa kabla yake ila saa moja tu ya mchana. Haya uliyo watolea waadhi yatosha. Hawataangamizwa kwa adhabu isipo kuwa walio toka kwenye ut'iifu.