Idd el-Hajj 2027

Tarehe inayotarajiwa

Jumapili, 16 Mei 2027

10 Dhul Hijja 1448 AH

Hadi Jumatano, 19 Mei 2027

Tarehe zinafuata kalenda ya Umm al-Qura ya Saudi Arabia. Mahali ambapo mwezi huanza kwa kuonekana kwa mwezi mwandamo katika eneo hilo, tarehe inaweza kuwa mapema au kuchelewa kwa siku moja.

Idd el-Hajj, Sikukuu ya Kuchinja, ni tarehe 10 Dhul Hijja. Waislamu huswali swala ya Idd kisha huchinja mnyama, wakimfuata Nabii Ibrahim. Siku tatu zinazofuata ni Siku za Tashriq.

Kutoka Qur'ani na Sunna

Hadithi

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: ضَحَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ أَقْرَنَيْنِ، ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ، وَسَمَّى وَكَبَّرَ، وَوَضَعَ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alichinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kondoo wawili wazuri weupe wenye pembe, aliwachinja kwa mkono wake, akasema, Bismillahi Allaahu Akbar, na akaweka mguu wake ubavuni mwao.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake · Sahihi
Maelezo

Ameeleza Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichinja kwa mkono wake siku ya Idil Adh-haa kondoo wawili madume wenye mapembe, weupe wenye mchanganyiko na weusi, na akasema: Bismillaahi wallaahu Akbaru, na akaweka mguu wake katika shingo zao.

Soma kwenye HadeethEnc.com

عَن أُمِّ سَلَمَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رضي الله عنها قَالت: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ كَانَ لَهُ ذِبْحٌ يَذْبَحُهُ فَإِذَا أُهِلَّ هِلَالُ ذِي الْحِجَّةِ، فَلَا يَأْخُذَنَّ مِنْ شَعْرِهِ، وَلَا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا حَتَّى يُضَحِّيَ».
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeandaa mnyama kwa ajili ya kuchinja, na ukaandama mwandamo wa mwezi Dhul Hija, basi asipunguze chochote katika nywele zake wala kucha zake mpaka atakapochinja mnyama wake wa Udh-hiya"
Imepokelewa Imamu Muslim · Sahihi
Maelezo

Amemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayetaka kuchinja Udh-hiya asipunguze chochote katika nywele za kichwa chake au kwapa yake au sharubu zake au zinginezo, wala sehemu ya kucha za mikono yake wala miguu yake utakapoonekana mwandamo wa Dhul-Hija mpaka atakapochinja.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Tazama pia

Miaka mingine

Matukio mengine

Maswali

Idd el-Hajj 2027 ni lini?

Idd el-Hajj 2027 inatarajiwa kuwa Jumapili, 16 Mei 2027, ambayo ni 10 Dhul Hijja 1448 AH kwa kalenda ya Umm al-Qura.

Je, tarehe ya Idd el-Hajj imethibitishwa?

Hapana, mpaka mwezi mwandamo uonekane. Nchi nyingi hutangaza mwanzo wa mwezi jioni ya kabla yake, kwa hiyo tarehe inaweza kusogea kwa siku moja.

Idd el-Hajj ni siku ngapi?

Idd el-Hajj ni tarehe 10 Dhul Hijja, na hufuatwa na Siku tatu za Tashriq, tarehe 11 hadi 13. Ni siku za kula na kumkumbuka Allah, si siku za funga ya Sunna.