Surat Yusuf, aya 78

12:78

قَالُواْ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡعَزِيزُ إِنَّ لَهُۥٓ أَبٗا شَيۡخٗا كَبِيرٗا فَخُذۡ أَحَدَنَا مَكَانَهُۥٓۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ٧٨

Qālū yā'ayyuhal-'azīzu inna lahū aban shaykhan kabīran fakhudh ahadanā makānahū innā narāka minal-muhsinīn

Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wema. 78

Maelezo ya chini

78 Wakawa hawana budi kujaribu kumvua ndugu yao au kumtolea fidia kwa kutaka kutimiza ile ahadi yao waliyo mpa Yaa'qub. Wakaingia kutaka kumlainisha moyo Yusuf kwa kumtajia uzee wa baba yao, wakamwambia: Ewe Mheshimiwa! Huyu ndugu yetu ana baba mtu mzima sana. Basi mfanyie huruma umchukue mmoja wetu mwenginewe awe badala ya mwanawe huyu ambaye ndiye anaye mpenda moyoni mwake. Matarajio yetu ni kuwa utatukubalia mambo yetu. Kwenu tumekwisha ona tabia yako ya ukarimu, na tumehakikisha mwendo wako wa kupenda kufanya hisani na kutenda mema.