قَالُواْ تَٱللَّهِ لَقَدۡ عَلِمۡتُم مَّا جِئۡنَا لِنُفۡسِدَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا كُنَّا سَٰرِقِينَ ٧٣
Qālū tallāhi laqad 'alimtum mā ji'nā linufsida fil-ardi wamā kunnā sāriqīn
Wakasema: Wallahi! Mnajua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi hii, wala sisi si wezi. 73
Maelezo ya chini
73 Nduguze Yusuf wakasema: Hakika kututuhumu sisi kwa wizi ni jambo la ajabu mno! Na tunahakikisha kwa kiapo ya kwamba nyinyi wenyewe mmeona katika mwendo wetu na tunavyo ishika dini yetu katika mara mbili tulipo kuja hapa kuwa mmejua yakini kuwa sisi hatutaki kuleta uharibifu katika nchi yenu. Wala si katika tabia yetu kuwa ni wezi.