Surat Yusuf, aya 46

12:46

يُوسُفُ أَيُّهَا ٱلصِّدِّيقُ أَفۡتِنَا فِي سَبۡعِ بَقَرَٰتٖ سِمَانٖ يَأۡكُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٞ وَسَبۡعِ سُنۢبُلَٰتٍ خُضۡرٖ وَأُخَرَ يَابِسَٰتٖ لَّعَلِّيٓ أَرۡجِعُ إِلَى ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَعۡلَمُونَ ٤٦

Yūsufu ayyuhas-siddīqu aftinā fī sab'i baqarātin simānin ya'kuluhunna sab'un 'ijāfun wasab'i sumbulātin khudrin wa ukhara yābisātil la'allī arji'u ilan-nāsi la'allahum ya'lamūn

Yusuf! Ewe mkweli! Tueleze nini maana ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba walio konda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa watu wapate kujua. 46

Maelezo ya chini

46 Yule mtumishi wa kumletea mfalme ulevi akenda kwa Yusuf, akamwita: Yusuf! Ewe uipendaye kweli! Tueleze nini maana ya ndoto ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe saba walio konda. Na ndoto ya mashuke saba mabichi na mengine makavu? Nataraji kurejea kwa watu nami nina fatwa yako, ili nao wapate kujua maana yake, na waujue ujuzi wako na fadhila yako.