Surat Yusuf, aya 40

12:40

مَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ أَسۡمَآءٗ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ ٤٠

Mā ta'budūna min dūnihī illā asmā'an sammaytumūhā antum wa ābā'ukum mā anzalallāhu bihā min sultānin inil-hukmu illā lillāhi amara allā ta'budū illā iyyāhu dhālikad-dīnul-qayyimu walākinna aktharan-nāsi lā ya'lamūn

Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui. 40

Maelezo ya chini

40 Hamuabudu badala ya Mwenyezi Mungu ila majina tu mliyo yazua nyinyi na baba zenu kwa mawazo bila ya kuwepo kweli. Mwenyezi Mungu hakuwateremshia hao hoja wala ushahidi wowote! Hapana wa kuhukumu nini kinacho faa kuabudiwa na kipi hakifai ila Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimnyenyekee yeyote mwenginewe, na mumuabudu Yeye peke yake. Hiyo ndiyo Dini iliyo nzima iliyo nyooka, ambayo dalili zote na ushahidi unaelekea kwake. Lakini aghlabu ya watu hawataki uwongozi wa dalili hizi, wala hawajijui kuwa wamo katika ujinga na upotovu.