قَالَتۡ فَذَٰلِكُنَّ ٱلَّذِي لُمۡتُنَّنِي فِيهِۖ وَلَقَدۡ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ فَٱسۡتَعۡصَمَۖ وَلَئِن لَّمۡ يَفۡعَلۡ مَآ ءَامُرُهُۥ لَيُسۡجَنَنَّ وَلَيَكُونٗا مِّنَ ٱلصَّٰغِرِينَ ٣٢
Qālat fadhālikunnal-ladhī lumtunnanī fīhi walaqad rāwattuhū 'an nafsihī fasta'sama wala'il lam yaf'al mā āmuruhū layusjananna walayakūnam minas-sāghirīn
Yule bibi akasema: Huyu basi ndiye huyo mliye nilaumia! Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa. Na akitofanya ninayo muamrisha basi hapana shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio chini kabisa. 32
Maelezo ya chini
32 Tena mke wa Mheshimiwa alisema kufuatiliza maneno yao: Huyu kijana ambaye uzuri wake umekuzugeni na ukakuemeeni hata yakatokea yaliyo tokea ndiye ambaye nyinyi mliye nilaumu kwa ajili yake! Na mimi kweli nilimtaka, na nikafanya juhudi kumghuri anikubalie, naye akajizuia na akakataa. Kama kwamba vile anavyo kataa ndio anazidi kumtia hamu yule mwanamke! Akasema mwanamke: Na mimi naapa! Kama hafanyi ninayo muamrisha atapata adhabu ya kifungo, na atakuwa katika madhalili wenye kudharauliwa!