فَلَمَّا ذَهَبُواْ بِهِۦ وَأَجۡمَعُوٓاْ أَن يَجۡعَلُوهُ فِي غَيَٰبَتِ ٱلۡجُبِّۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمۡرِهِمۡ هَٰذَا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ١٥
Falammā dhahabū bihī wa ajma'ū an yaj'alūhu fī ghayābatil-jubbi wa awhaynā ilayhi latunabbi'annahum bi amrihim hādhā wahum lā yash'urūn
Basi walipo mchukua na wakakubaliana wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hapana shaka yoyote utakuja waambia kwa jambo lao hili, na wala wao hawatambui. 15
Maelezo ya chini
15 Walipo kwenda naye mbali na baba yake, na wakakubaliana rai yao ya kumtumbukiza ndani ya kisima, walifanya hayo waliyo yaazimia. Sisi tukamtia moyoni mwake Yusuf atulie, na awe na imani ya Mwenyezi Mungu, kuwa bila ya shaka atakuja waeleza haya mambo yao waliyo yapanga na wakayatenda, na wala wao wenyewe hawajui hapo utapo waambia kwamba wewe ndiye Yusuf waliye mfanyia vitimbi, na wakadhani wamekwisha mmaliza na wameepukana naye!