Surat Yusuf, aya 11

12:11

قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأۡمَ۬نَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُۥ لَنَٰصِحُونَ ١١

Qālū yā'abānā mā laka lā ta'mannā 'alā yūsufa wa innā lahū lanāsihūn

Wakasema: Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na hakika sisi ni wenye kumtakia kheri! 11

Maelezo ya chini

11 Baada ya kuwafikiana kumbaidisha Yusuf (kumpeleka mbali) walisema: Ewe baba yetu! Nini kinacho kutia shaka nasi hata unamtenga Yusuf nasi, wala huoni pana usalama anapo kuwa nasi? Sisi tunakuhakikishia kuwa sisi tunampenda, na tunamwonea huruma, na tunamtakia kheri, na tunamwongoza kwenye kheri. Hapati kwetu isipo kuwa mahaba, na nasiha safi kabisa.