Surat Yunus, aya 93

10:93

وَلَقَدۡ بَوَّأۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ مُبَوَّأَ صِدۡقٖ وَرَزَقۡنَٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ فَمَا ٱخۡتَلَفُواْ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقۡضِي بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ ٩٣

Walaqad bawwa'nā banī isrā'īla mubawwa'a sidqin warazaqnāhum minat-tayyibāti famakhtalafū hattā jā'ahumul-'ilmu inna rabbaka yaqdī baynahum yawmal-qiyāmati fīmā kānū fīhi yakhtalifūn

Na hakika tuliwaweka Wana wa Is raili kikao chema, na tukawaruzuku vitu vizuri. Nao hawakukhitalifiana mpaka ilipo wafikia ilimu. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana. 93

Maelezo ya chini

93 Na tuliwaweka vyema Wana wa Israili wakaishi katika nchi nzuri na huku wakiihifadhi Dini yao, nao wako mbali na dhulma iliyo kuwa ikiwapata; riziki na neema zimewajalia. Lakini mara baada ya kuonja neema ya utukufu baada ya unyonge, yaliwasibu maradhi ya kufarikiana. Wakakhitalifiana juu ya kuwa imekwisha bainika kweli na uwongo! Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao Siku ya Kiyama, na atamlipa kila mmoja kwa alilo tenda.