Surat Yunus, aya 79

10:79

وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ ٱئۡتُونِي بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ ٧٩

Waqāla fir'awnu'tūnī bikulli sāhirin 'alīm

Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi mjuzi! 79

Maelezo ya chini

79 Firauni na kaumu yake wakadai kuwa Musa na nduguye ni wachawi, wala si Mitume! Akawataka watu wake wamhudhurishe kila aliye hodari katika fani za uchawi katika mamlaka yake.