Surat Yunus, aya 78

10:78

قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِتَلۡفِتَنَا عَمَّا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا ٱلۡكِبۡرِيَآءُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا نَحۡنُ لَكُمَا بِمُؤۡمِنِينَ ٧٨

Qālū aji'tanā litalfitanā 'ammā wajadnā 'alayhi ābā'anā watakūna lakumal-kibriyā'u fil-ardi wamā nahnu lakumā bimu'minīn

Wakasema: Je! Umetujia ili utuachishe tuliyo wakuta nayo baba zetu, na mpate nyinyi wawili ukubwa katika nchi? Wala sisi hatukuaminini nyinyi. 78

Maelezo ya chini

78 Firauni na watu wake walimwambia Musa: Hapana shaka wewe umekuja kwa makusudi ya kutuachisha dini ya baba zetu, na mila za kaumu yetu, ili nyinyi wawili mpate kuwa na wafuasi; wewe na nduguyo mpate ufalme na utukufu na urais wa kutawala na kuhukumu! Kwa hivyo basi sisi hatutakuaminini nyinyi wala huo utume wenu!