مَتَٰعٞ فِي ٱلدُّنۡيَا ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ ٱلۡعَذَابَ ٱلشَّدِيدَ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ ٧٠
Matā'un fid-dunyā thumma ilaynā marji'uhum thumma nudhīquhumul-'adhābash-shadīda bimā kānū yakfurūn
Hiyo ni starehe ya katika dunia tu, kisha marejeo yao ni kwetu. Tena tutawaonjesha adhabu kali kwa sababu ya kukufuru kwao. 70
Maelezo ya chini
70 Wao wana starehe hapa duniani ya kudanganyika nayo. Nayo ni chache, ikiwa itachukua muda mrefu au mfupi, ukilinganisha na hayo yanayo wangojea! Kisha marejeo yao ni kwetu, Sisi. Tutawahisabia na tutawaonjesha adhabu ya kutia uchungu kwa sababu ya ukafiri wao.