قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ ٣٤
Qul hal min shurakā'ikum man yabda'ul-khalqa thumma yu'īduhū qulillāhu yabda'ul-khalqa thumma yu'īduhū fa annā tu'fakūn
Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina aliye anzisha kuumba viumbe, na kisha akavirejesha? Huwaje, basi, mkadanganywa? 34
Maelezo ya chini
34 Ewe Mtume! Waambie hao washirikina: Yupo yeyote katika hao mlio wafanya washirika wa Mwenyezi Mungu mkawaabudu, awezaye kuanzisha kuumba tangu mwanzo, na tena akarejea tena baada ya kwisha toweka? Hapana shaka watashindwa kujibu! Basi hapo tena waambie: Allah, Mwenyezi Mungu, tu peke yake, ndiye anaye anzisha kuumba kutokana na kuto kuwepo, na tena viumbe vikitoweka huvirejesha. Vipi basi nyinyi mnaiacha Imani?