كَذَٰلِكَ حَقَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى ٱلَّذِينَ فَسَقُوٓاْ أَنَّهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ ٣٣
Kadhālika haqqat kalimatu rabbika 'alal-ladhīna fasaqū annahum lā yu'minūn
Ndio kama hivyo kauli ya Mola wako Mlezi itakavyo wathibitikia wale walio potoka, ya kwamba hawatoamini. 33
Maelezo ya chini
33 Kama ulivyo thibiti Ungu wa Mwenyezi Mungu na kumuabudu Yeye, vile vile imethibiti hukumu juu ya walio tokana na amri ya Mwenyezi Mungu wakimuasi kwa kuwa hawaifuati Haki. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hawaongoi kwenye Haki ila wanao ishika njia yake, sio wanao mfanyia uasi.