قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ ٧٦
Qāla ana khayrum minhu khalaqtanī min nārin wakhalaqtahū min tīn
Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. 76
Maelezo ya chini
76 Iblisi akasema: Mimi ni bora kuliko Adam; kwani Wewe umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. Basi vipi mimi nimsujudie yeye?