وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ بَلۡ مَكۡرُ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ إِذۡ تَأۡمُرُونَنَآ أَن نَّكۡفُرَ بِٱللَّهِ وَنَجۡعَلَ لَهُۥٓ أَندَادٗاۚ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۚ وَجَعَلۡنَا ٱلۡأَغۡلَٰلَ فِيٓ أَعۡنَاقِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۖ هَلۡ يُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٣٣
Waqālal-ladhīnastud'ifū lilladhīnastakbarū bal makrul-layli wan-nahāri idh ta'murūnanā an nakfura billāhi wanaj'ala lahū andādan wa asarrun-nadāmata lammā ra'awul-'adhāba waja'alnal-aghlāla fī a'nāqil-ladhīna kafarū hal yujzawna illā mā kānū ya'malūn
Na wanyonge wakawaambia walio takabari: Bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipo kuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie washirika. Nao wataficha majuto watakapo iona adhabu. Na tutaweka makongwa shingoni mwao walio kufuru. Kwani wanalipwa ila kwa waliyo kuwa wakiyatenda? 33
Maelezo ya chini
33 Na wanyonge nao watawaambia walio takabari: Bali vitimbi vyenu na uchochezi wenu kutuchochea usiku na mchana ndio umetutumbukiza katika hilaki, pale mlipo kuwa mkitutaka tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie miungu mingine ya kumshirikisha. Na pande zote mbili zikaficha majuto yao walipo iona adhabu inawashukia. Wakajua kuwa hapana faida ya kuonyesha majuto. Na tukayaweka makongwa, (nira), juu ya shingo za wasio amini. Je! Watu hawa wanastahiki chochote ila malipo kwa yale waliyo kuwa wakiyatenda?