Surat Saba, aya 13

34:13

يَعۡمَلُونَ لَهُۥ مَا يَشَآءُ مِن مَّحَٰرِيبَ وَتَمَٰثِيلَ وَجِفَانٖ كَٱلۡجَوَابِ وَقُدُورٖ رَّاسِيَٰتٍۚ ٱعۡمَلُوٓاْ ءَالَ دَاوُۥدَ شُكۡرٗاۚ وَقَلِيلٞ مِّنۡ عِبَادِيَ ٱلشَّكُورُ ١٣

Ya'malūna lahū mā yashā'u mim mahārība watamāthīla wajifānin kal-jawābi waqudūrir rāsiyātini'malū āla dāwūda shukran waqalīlum min 'ibādiyash-shakūr

Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyo ondolewa mahala pake. Enyi watu wa Daudi! Fanyeni kazi kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanao shukuru. 13

Maelezo ya chini

13 Hao majini wakifanya atakacho Suleiman, kama misikiti kwa ajili ya ibada, na masanamu, na madeste au mabakuli makubwa kama mahodhi ya maji, na vyombo vya kupikia, yaani masufuria, makubwa yaliyo kaa pale pale penye mafya yake hayaondoki kwa kuwa ni makubwa mno. Na tukawaambia watu wa Daudi: Tendeni kazi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu vilivyo. Na ni wachache miongoni mwa waja wangu ambao wanakumbuka neema zangu wakawa wananishukuru kwa wingi.