أَنِ ٱعۡمَلۡ سَٰبِغَٰتٖ وَقَدِّرۡ فِي ٱلسَّرۡدِۖ وَٱعۡمَلُواْ صَٰلِحًاۖ إِنِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ١١
Ani'mal sābighātin waqaddir fis-sardi wa'malū sālihan innī bimā ta'malūna basīr
(Tukamwambia:) Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayo yatenda. 11
Maelezo ya chini
11 Tulimfunulia kumwambia aunde nguo za chuma pana za kujilinda katika vita na maadui. Naye azifume kwa hikima na ustadi katika kuviunga viungo vyake. Na tukamwambia yeye na watu wake: Tendeni yatakayo kuleteeni kheri na maslaha. Hakika Mimi nayaona vyema yote myatendayo, hapana kinacho niporonyoka nisikione.