Rabbana la tuzigh qulubana

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

3:8

رَبَّنَا لَا تُزِغۡ قُلُوبَنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَيۡتَنَا وَهَبۡ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحۡمَةًۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡوَهَّابُ ٨

Rabbanā lā tuzigh qulūbanā ba'da idh hadaytanā wahab lanā mil ladunka rahmatan innaka antal-wahhāb

(Na hao husema): Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji. 8

Maelezo ya chini

8 Hao wanazuoni wenye akili husema: Mola wetu Mlezi! Usizifanye nyoyo zetu zikaacha Haki baada ya Wewe kwisha tuongoza kuiendea hiyo Haki. Ewe Mola wetu Mlezi! Tupe rehema kutoka kwako kwa kutuwezesha na kututhibitisha. Hakika Wewe ndiwe Mwenye kunyima na ndiwe Mpaji.

3:9

رَبَّنَآ إِنَّكَ جَامِعُ ٱلنَّاسِ لِيَوۡمٖ لَّا رَيۡبَ فِيهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ ٩

Rabbanā innaka jāmi'un-nāsi liyawmil lā rayba fīhi innallāha lā yukhliful-mī'ād

Mola wetu Mlezi! Wewe ndiye Mkusanyaji wa watu kwa Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake. 9

Maelezo ya chini

9 Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ndiwe utao wakusanya watu Siku hiyo isiyo na shaka, ili kumlipa kila mmojapo kwa alilo litenda. Kwani Wewe umeahidi hayo, na Wewe hukhalifu miadi yako.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Al-Imran yote

Maswali

Rabbana la tuzigh qulubana iko wapi katika Qur'ani?

Rabbana la tuzigh qulubana iko katika Surat Al-Imran, 3:8-9.