۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَلَا تُبۡطِلُوٓاْ أَعۡمَٰلَكُمۡ ٣٣
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū atī'ullāha wa atī'ur-rasūla walā tubtilū a'mālakum
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu. 33
Maelezo ya chini
33 Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu katika aliyo kuamrisheni, na mt'iini Mtume kwa hayo anayo kuitieni, wala msivipoteze vitendo vyenu.