Surat Muhammad, aya 20

47:20

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَوۡلَا نُزِّلَتۡ سُورَةٞۖ فَإِذَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ مُّحۡكَمَةٞ وَذُكِرَ فِيهَا ٱلۡقِتَالُ رَأَيۡتَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ نَظَرَ ٱلۡمَغۡشِيِّ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡمَوۡتِۖ فَأَوۡلَىٰ لَهُمۡ ٢٠

Wayaqūlul-ladhīna āmanū lawlā nuzzilat sūratun fa idhā unzilat sūratum muhkamatun wadhukira fīhal-qitālu ra'aytal-ladhīna fī qulūbihim maradun yanzurūna ilayka nazaral-maghshiyyi 'alayhi minal-mawti fa awlā lahum

Na Waumini wanasema: Kwa nini haiteremshwi Sura? Na inapo teremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake khabari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anaye zimia kwa mauti. Basi ni bora kwao 20

Maelezo ya chini

20 Walio amini wanasema: Haiteremki Sura ya kututaka tupigane? Na ikiteremka Sura ambayo haifasiriki vyenginevyo ila ni kulazimisha tu, na ikataja ndani yake kuamrishwa vita, utawaona ambao katika nyoyo zao mna unaafiki wanakuangalia kwa muangalio wa mwenye kuzimia kwa mauti, jinsi ya kuviogopa na kuvichukia vita. Linalo wastahikia kulifanya ni kumt'ii Mwenyezi Mungu na kusema neno linalo kubaliana na sharia.