مَّثَلُ ٱلۡجَنَّةِ ٱلَّتِي وُعِدَ ٱلۡمُتَّقُونَۖ فِيهَآ أَنۡهَٰرٞ مِّن مَّآءٍ غَيۡرِ ءَاسِنٖ وَأَنۡهَٰرٞ مِّن لَّبَنٖ لَّمۡ يَتَغَيَّرۡ طَعۡمُهُۥ وَأَنۡهَٰرٞ مِّنۡ خَمۡرٖ لَّذَّةٖ لِّلشَّٰرِبِينَ وَأَنۡهَٰرٞ مِّنۡ عَسَلٖ مُّصَفّٗىۖ وَلَهُمۡ فِيهَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ وَمَغۡفِرَةٞ مِّن رَّبِّهِمۡۖ كَمَنۡ هُوَ خَٰلِدٞ فِي ٱلنَّارِ وَسُقُواْ مَآءً حَمِيمٗا فَقَطَّعَ أَمۡعَآءَهُمۡ ١٥
Mmathalul-jannatil-latī wu'idal-muttaqūna fīhā anhārum mim mā'in ghayri āsinin wa anhārum mil labanil lam yataghayyar ta'muhū wa anhārum min khamril laddhatil lish-shāribīna wa anhārum min 'asalim musaffan walahum fīhā min kullith-thamarāti wamaghfiratum mir rabbihim kaman huwa khālidun fin-nāri wasuqū mā'an hamīman faqatta'a am'ā'ahum
Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao? 15
Maelezo ya chini
15 Sifa ya Pepo walio ahidiwa wachamngu ni kama hivi: ndani yake imo mito ya maji yasiyo chafuka, na mito ya maziwa yasiyo haribika utamu wake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa na takataka zote. Na humo watakuwa na kila namna ya matunda, na msamaha mkubwa kutokana na Mola wao Mlezi. Je! Sifa za Pepo ya hawa ni kama sifa itayo kuwa ni malipo ya mwenye kudumu milele Motoni, na akanyweshwa maji yaliyo tokota ya kukata matumbo? Aya hii tukufu inataka tuzingatie kuwa maji yaliyo vunda, yaliyo tuama, yenye kutaghayari, ni maji yenye madhara. Na Aya hii tukufu imesema hayo kabla ya kuvumbuliwa darubini za kutazamia vijidudu (Microscope) kwa makarne ya miaka, ndipo ilipo juulikana kuwa maji yaliyo tuama yaliyo taghayari yanakuwamo ndani yake mamilioni ya vijidudu vyenye madhara ya kuwasibu watu na wanyama kwa namna mbali mbali ya magonjwa.