وَإِذَا غَشِيَهُم مَّوۡجٞ كَٱلظُّلَلِ دَعَوُاْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ فَلَمَّا نَجَّىٰهُمۡ إِلَى ٱلۡبَرِّ فَمِنۡهُم مُّقۡتَصِدٞۚ وَمَا يَجۡحَدُ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَّا كُلُّ خَتَّارٖ كَفُورٖ ٣٢
Wa idhā ghashiyahum mawjun kaz-zulali da'awullāha mukhlisīna lahud-dīna falammā najjāhum ilal-barri faminhum muqtasidun wamā yajhadu bi'āyātinā illā kullu khattārin kafūr
Na wimbi linapo wafunika kama wingu, wao humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapo waokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa sawa. Wala hazikanushi Ishara zetu ila aliye khaini kafiri mkubwa. 32
Maelezo ya chini
32 Hawa makafiri wanao mkataa Mwenyezi Mungu wakipanda marikebu, na bahari ikawachafukia, na mawimbi yakaja juu mpaka wakaona yatawafunika, na wakawa yakini watazama bila ya muhali, humkimbilia Mwenyezi Mungu, wakimwomba kwa ikhlasi na unyenyekevu, awaokoe. Basi akisha waokoa wakafika nchi kavu wapo kati yao wachache wanao kumbuka ahadi yao, na wakenda mwendo wa sawa. Na wapo kati yao, nao ndio wengi, walio sahau fadhila za Mola wao Mlezi, na wakaendelea na kumkataa. Na wala hakatai fadhila za Mola wake Mlezi na hisani yake ila kila mtu aliye mwingi wa ukhaini, aliye pita mpaka kumkanya Mola wake Mlezi.