Surat Ibrahim, aya 8

14:8

وَقَالَ مُوسَىٰٓ إِن تَكۡفُرُوٓاْ أَنتُمۡ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا فَإِنَّ ٱللَّهَ لَغَنِيٌّ حَمِيدٌ ٨

Waqāla mūsā in takfurū antum waman fil-ardi jamī'an fa innallāha laghaniyyun hamīd

Na Musa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote waliomo duniani, hakika Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Anajitosha, Msifiwa. 8

Maelezo ya chini

8 Na Musa aliwaambia watu wake walipo mpinga na kumkanya: Mkizikanya neema za Mwenyezi Mungu, wala msishukuru kwa Imani na ut'iifu, nyinyi na wote waliomo duniani, basi hakika hayo hayatamdhuru Mwenyezi Mungu chochote. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, hahitajii shukra za wanao shukuru. Yeye ni Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa dhati yake, bila ya yeyote kumhimidi.