وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ غَٰفِلًا عَمَّا يَعۡمَلُ ٱلظَّٰلِمُونَۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمۡ لِيَوۡمٖ تَشۡخَصُ فِيهِ ٱلۡأَبۡصَٰرُ ٤٢
Walā tahsabannallāha ghāfilan 'ammā ya'maluz-zālimūna innamā yu'akkhiruhum liyawmin tashkhasu fīhil-absār
Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao. 42
Maelezo ya chini
42 Ewe Mtume! Wala usidhani kabisa kuwa Mola wako Mlezi ameghafilika na vitendo wafanyavyo wenye kudhulumu, kuupiga vita Uislamu na Waislamu wenyewe. Bali Yeye anaujua ukhalifu wao. Na amekadiria kuakhirisha kuwaadhibu mpaka Siku nzito. Macho yao yatabaki yamekodoka, hawawezi kuyafumba, wala kupepesa kwa kitisho watacho kiona.