Surat Ibrahim, aya 38

14:38

رَبَّنَآ إِنَّكَ تَعۡلَمُ مَا نُخۡفِي وَمَا نُعۡلِنُۗ وَمَا يَخۡفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ ٣٨

Rabbanā innaka ta'lamu mā nukhfī wamā nu'linu wamā yakhfā 'alallāhi min shay'in fil-ardi walā fis-samā'

Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe unajua tunayo yaficha na tunayo yatangaza. Na hapana kitu kinacho fichikana kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika mbingu. 38

Maelezo ya chini

38 Ewe Mola wetu Mlezi! Ni sawa sawa kwako tunayo fanya siri na tunayo fanya dhaahiri. Kwani Wewe unajua maslaha yetu, na unatuonea huruma zaidi kuliko sisi wenyewe. Na hapana lifichikanalo kwako hata likiwa dogo, katika ardhi na katika mbingu. Basi hapana haja sisi ya kukuomba. Lakini juu ya hivyo tunaomba kwa kuonyesha kuwa sisi ni waja wako, twanyenyekea utukufu wako, na tunahitajia uliyo nayo, Wewe!