Surat Ibrahim, aya 37

14:37

رَّبَّنَآ إِنِّيٓ أَسۡكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيۡرِ ذِي زَرۡعٍ عِندَ بَيۡتِكَ ٱلۡمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱجۡعَلۡ أَفۡـِٔدَةٗ مِّنَ ٱلنَّاسِ تَهۡوِيٓ إِلَيۡهِمۡ وَٱرۡزُقۡهُم مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَشۡكُرُونَ ٣٧

Rrabbanā innī askantu min dhurriyyatī biwādin ghayri dhī zar'in 'inda baytikal-muharrami rabbanā liyuqīmus-salawāta faj'al af'idatam minan-nāsi tahwī ilayhim warzuqhum minath-thamarāti la'allahum yashkurūn

Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuriya zangu katika bonde lisilo kuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili washike Swala. Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku matunda, ili wapata kushukuru. 37

Maelezo ya chini

37 Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika mimi nimewafanyia maskani baadhi ya dhuriya zangu katika bonde la Makka ambalo halioti mimea, kwenye Nyumba yako uliyo kataza isiingiliwe na kuvunjiwa hishima yake, na ukajaalia sehemu za jirani yake ziwe na amani. Ewe Mola wetu Mlezi! Wakirimu wapate kushika Swala karibu na Nyumba hii. Na zijaalie nyoyo za bora ya watu ziwapende kwa kuizuru Nyumba yako. Na uwaruzuku matunda kwa kuletwa na hao watakao kuja, ili wapate kushukuru neema yako kwa Swala na Dua.