Surat Ibrahim, aya 32

14:32

ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزۡقٗا لَّكُمۡۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡفُلۡكَ لِتَجۡرِيَ فِي ٱلۡبَحۡرِ بِأَمۡرِهِۦۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡأَنۡهَٰرَ ٣٢

Allāhul-ladhī khalaqas-samāwāti wal-arda wa anzala minas-samā'i mā'an fa akhraja bihī minath-thamarāti rizqal lakum wasakkhara lakumul-fulka litajriya fil-bahri bi amrihī wasakkhara lakumul-anhār

Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito ikutumikieni. 32

Maelezo ya chini

32 Ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye zianzisha mbingu na viliomo ndani yake, na ardhi na viliomo ndani yake. Na akateremsha kutoka mawinguni maji ya kumiminika. Na kwa sababu yake akakutoleeni riziki ya matunda, na mazao mengine na miti. Na Yeye akakufanyieni vyombo vya baharini vikufaeni vinakwenda na kupakia riziki zenu, na bidhaa zenu za biashara, kwa idhini yake na kutaka kwake. Na akaifanya mito ya maji matamu ikunufaisheni kwa kunywa nyinyi na kumwagia katika mashamba yenu.