Surat Ibrahim, aya 30

14:30

وَجَعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادٗا لِّيُضِلُّواْ عَن سَبِيلِهِۦۗ قُلۡ تَمَتَّعُواْ فَإِنَّ مَصِيرَكُمۡ إِلَى ٱلنَّارِ ٣٠

Waja'alū lillāhi andādal liyudillū 'an sabīlihī qul tamatta'ū fa inna masīrakum ilan-nār

Na walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili wapoteze watu kwenye Njia yake. Sema: Stareheni! Kwani marejeo yenu ni Motoni! 30

Maelezo ya chini

30 Na wakamfanyia Mwenyezi Mungu Mmoja wa pekee mifano ya masanamu wakiyaabudu, kwa ajili ya kuwa natija ya vitendo vyao iwe kuwapoteza watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu! Ewe Nabii! Waambie hao walio potea: Stareheni na matamanio yenu, kwani marejeo yenu ni Motoni!