Surat Hud, aya 89

11:89

وَيَٰقَوۡمِ لَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شِقَاقِيٓ أَن يُصِيبَكُم مِّثۡلُ مَآ أَصَابَ قَوۡمَ نُوحٍ أَوۡ قَوۡمَ هُودٍ أَوۡ قَوۡمَ صَٰلِحٖۚ وَمَا قَوۡمُ لُوطٖ مِّنكُم بِبَعِيدٖ ٨٩

Wayāqawmi lā yajrimannakum shiqāqī an yusībakum mithlu mā asāba qawma nūhin aw qawma hūdin aw qawma sālihin wamā qawmu lūtim minkum biba'īd

Na enyi watu wangu! Kukhalifiana nami kusikupelekeeni hata mkasibiwa kama walivyo sibiwa watu wa Nuhu, au watu wa Hud, au watu wa Saleh. Na watu wa Lut' si mbali nanyi. 89

Maelezo ya chini

89 Na enyi watu! Hizi khitilafu ziliopo baina yangu na nyinyi zisikupelekeeni kufanya inda na mkashikilia ukafiri, hata yakakupateni yaliyo wapata kaumu ya Nuhu, na kaumu ya Huud, na kaumu ya Swaleh. Na wala zama na pahala pa kaumu Lut' na maangamizo yao si mbali nanyi! Basi zingatieni yasikusibuni yaliyo wasibu hao.