Surat Hud, aya 73

11:73

قَالُوٓاْ أَتَعۡجَبِينَ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۖ رَحۡمَتُ ٱللَّهِ وَبَرَكَٰتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِۚ إِنَّهُۥ حَمِيدٞ مَّجِيدٞ ٧٣

Qālū ata'jabīna min amrillāhi rahmatullāhi wabarakātuhū 'alaykum ahlal-bayti innahū hamīdum majīd

Wakasema: Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ndiye Msifiwa wa kutukuzwa. 73

Maelezo ya chini

73 Malaika wakamwambia: Unastaajabu nyinyi wawili kupata mwana kwa ajili ya uzee wenu? Haya yanatokana na amri ya Mwenyezi Mungu asiye shindwa na chochote. Hiyo ndiyo rehema ya Mwenyezi Mungu. Na neema zake ni nyingi juu yenu wa ukoo wa Nabii. Basi hapana la ajabu nyinyi kupewa wasio pewa wenginewe. Mwenye kutenda hayo hakika anastahiki kuhimidiwa, ni mwingi wa hisani na ukarimu na upaji.