مِن دُونِهِۦۖ فَكِيدُونِي جَمِيعٗا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ ٥٥
Min dūnihī fakīdūnī jamī'an thumma lā tunzirūn
Mkamwacha Yeye. Basi nyote nyinyi nipangieni vitimbi, na kisha msinipe muhula! 55
Maelezo ya chini
55 Wala mimi sikujalini, wala siwajali miungu yenu hiyo ambayo mnadai kuwa imenipatiliza kwa uovu! Basi saidianeni, nyinyi na miungu yenu, kunifanyia vitimbi. Kisha wala msiakhirishe hiyo adhabu yenu kwangu hata dakika moja, kama mnaweza!