إِن نَّقُولُ إِلَّا ٱعۡتَرَىٰكَ بَعۡضُ ءَالِهَتِنَا بِسُوٓءٖۗ قَالَ إِنِّيٓ أُشۡهِدُ ٱللَّهَ وَٱشۡهَدُوٓاْ أَنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ ٥٤
In naqūlu illa'tarāka ba'du ālihatinā bisū'in qāla innī ushhidullāha washhadū annī barī'um mimmā tushrikūn
Sisi tunasema: Baadhi katika miungu yetu imekusibu kwa baa. Akasema: Hakika mimi namshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi najitenga mbali na hao mnao wafanya washirika, 54
Maelezo ya chini
54 Na hatuna la kusema juu ya msimamo wako nasi ila kuwa mmojapo katika miungu yetu imekupatiliza kwa shari, ndio maana ukawa unaropokwa maneno haya! Naye akasema naye ameshikilia Imani yake na anawapinga: Ninasema, na namshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa haya niyasemayo, na nakushuhudisheni nyinyi, ya kwamba mimi najitenga mbali kabisa na maradhi ya ushirikina mliyo nayo. Kwani nyinyi ni wagonjwa!