وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۖ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا مُفۡتَرُونَ ٥٠
Wa ilā 'ādin akhāhum hūdan qāla yāqawmi'budullāha mā lakum min ilāhin ghayruhū in antum illā muftarūn
Na kwa kina A'adi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Nyinyi hamna mungu isipo kuwa Yeye. Nyinyi si chochote ila ni wazushi tu. 50
Maelezo ya chini
50 Na Sisi tuliwapelekea Kaumu ya A'adi wa mwanzo ndugu yao katika kabila yao, naye ni huyo Huud. Akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu pekee. Kwani hamna anaye stahiki kuabudiwa isipo kuwa Yeye. Na nyinyi si cho chote ila mnazua uwongo tu kudai kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika wanao stahiki nao kuabudiwa ili wawe waombezi wenu kwa Mwenyezi Mungu! Tazama maelezo ya ki-ilimu juu ya Aya 65 katika Sura Al-Aa'raaf. (7).