Surat Hud, aya 41

11:41

۞ وَقَالَ ٱرۡكَبُواْ فِيهَا بِسۡمِ ٱللَّهِ مَجۡر۪ىٰهَا وَمُرۡسَىٰهَآۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ ٤١

Waqālarkabū fīhā bismillāhi majrāhā wamursāhā inna rabbī laghafūrur rahīm

Na akasema: Pandeni humo kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. 41

Maelezo ya chini

41 Na baada ya kwisha liweka tayari jahazi Nuhu aliwaambia watu wake: Pandeni humo kwa kujipigia feli njema kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu (kupiga BISMILLAHI) wakati wa kwenda na wakati wa kusimama, na wakati wa kuingia na wakati wa kutoka humo. Na muombeni Mwenyezi Mungu akusameheni kwa madhambi mlio tenda, na akurehemuni. Kwani maghfira na rehema ni katika shani yake Subhanahu wa Taa'la.