وَيَٰقَوۡمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِن طَرَدتُّهُمۡۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ٣٠
Wayāqawmi man yansurunī minallāhi in tarattuhum afalā tadhakkarūn
Na enyi watu wangu! Ni nani atakaye nisaidia kwa Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hawa? Basi je, hamfikiri? 30
Maelezo ya chini
30 Enyi watu! Hapana yeyote awezaye kunikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu nikiwafukuza hao hali nao ni wenye kumuamini Yeye. Je, bado mngali mnashikilia ujinga wenu? Hamkumbuki basi kuwa hawa watu wanaye Mola wao Mlezi wa kuwalipia?