قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي رَحۡمَةٗ مِّنۡ عِندِهِۦ فَعُمِّيَتۡ عَلَيۡكُمۡ أَنُلۡزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمۡ لَهَا كَٰرِهُونَ ٢٨
Qāla yāqawmi ara'aytum in kuntu 'alā bayyinatim mir rabbī wa ātānī rahmatam min 'indihī fa'ummiyat 'alaykum anulzimukumūhā wa antum lahā kārihūn
Akasema: Enyi watu wangu! Hebu fikirini! Ikiwa mimi ninayo hoja wazi iliyo toka kwa Mola wangu Mlezi, na amenipa rehema kutoka kwake, nayo ikakufichikieni; je, tukulazimisheni kuikubali hali nyinyi mnaichukia? 28
Maelezo ya chini
28 Nuhu akasema: Enyi watu! Hebu nambieni, ikiwa mimi naungwa mkono na hoja zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akanipa kwa rehema yake Unabii na Utume, na nuru yake ikafichikana kwenu, na kughurika kwenu kwa cheo na mali kukakutieni upofu msizione, basi je, itafaa tukulazimisheni mziamini hoja kwa nguvu na karaha?