مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيۡهِمۡ أَعۡمَٰلَهُمۡ فِيهَا وَهُمۡ فِيهَا لَا يُبۡخَسُونَ ١٥
Man kāna yurīdul-hayawātad-dunyā wazīnatahā nuwaffi ilayhim a'mālahum fīhā wahum fīhā lā yubkhasūn
Wanao taka maisha ya dunia na pumbao lake tutawalipa humo vitendo vyao kaamili. Na wao humo hawatopunjwa. 15
Maelezo ya chini
15 Wenye kutaka uhai wa duniani, na kustarehea ladha zake na pumbao lake, tutawapa matunda ya vitendo vyao bila ya nuksani.