Surat Hud, aya 14

11:14

فَإِلَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَآ أُنزِلَ بِعِلۡمِ ٱللَّهِ وَأَن لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَهَلۡ أَنتُم مُّسۡلِمُونَ ١٤

Fa illam yastajībū lakum fa'lamū annamā unzila bi'ilmillāhi wa al lā ilāha illā huwa fahal antum muslimūn

Na wasipo kuitikieni, basi jueni ya kwamba (hii Qur'ani) imeteremshwa kwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hapana mungu ila Yeye. Basi je! Nyinyi ni Waislamu? 14

Maelezo ya chini

14 Mkishindwa, na wakashindwa mlio wataka msaada, kuleta mfano wake hii wa kuzua, basi jueni kuwa Qur'ani haikuteremshwa ila kwa kuambatana na ujuzi wake Mwenyezi Mungu. Ilimu yake haijui mtu ila Yeye. Na jueni kuwa hapana mungu ila Allah, Mwenyezi Mungu tu. Hapana anaye tenda kazi yake. Basi kuweni Waislamu baada ya kwisha thibiti hoja hizi juu yenu, kama nyinyi mnataka Haki.