Surat Hud, aya 116

11:116

فَلَوۡلَا كَانَ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِن قَبۡلِكُمۡ أُوْلُواْ بَقِيَّةٖ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡفَسَادِ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّنۡ أَنجَيۡنَا مِنۡهُمۡۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَآ أُتۡرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجۡرِمِينَ ١١٦

Falawlā kāna minal-qurūni min qablikum ulū baqiyyatin yanhawna 'anil-fasādi fil-ardi illā qalīlam mimman anjaynā minhum wattaba'al-ladhīna zalamū mā utrifū fīhi wakānū mujrimīn

Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao, na wakawa ni wakosefu. 116

Maelezo ya chini

116 Ilikuwa inapasa katika kaumu zilizo tangulia na tukaziteketeza kwa dhulma zao, wawepo jamaa kati yao wenye kusikilizwa kauli yao, na wenye vyeo katika dini na akili, wawakanye wenzi wao waache uharibifu katika nchi, ili wasalimike na adhabu iliyo wateremkia. Lakini hayakuwa hayo. Yaliyo tokea ni kuwa walikuwapo Waumini wachache wasio sikilizwa rai zao wala uwongozi wao. Hao Mwenyezi Mungu aliwaokoa pamoja na Mitume wao wakati ule walipo shikilia wenye kudhulumu wenye inda kung'ang'anilia yale maisha ya anasa na fisadi waliyo yazoea. Hayo yakawa ni pingamizi wasiweze kunafiika na wito wa Haki na kheri, na kwa kukhiari kwao njia hiyo wakazama katika madhambi na vitendo viovu. Basi Mwenyezi Mungu akawahiliki kwa mujibu wa mwendo wake wa maumbile.