فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّمَّا يَعۡبُدُ هَٰٓؤُلَآءِۚ مَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُهُم مِّن قَبۡلُۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمۡ نَصِيبَهُمۡ غَيۡرَ مَنقُوصٖ ١٠٩
Falā taku fī miryatim mimmā ya'budu hā'ulā'i mā ya'budūna illā kamā ya'budu ābā'uhum min qablu wa innā lamuwaffūhum nasībahum ghayra manqūs
Basi usiwe na shaka juu ya wanayo yaabudu hao. Hawaabudu ila kama walivyo abudu baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa. 109
Maelezo ya chini
109 Ilivyo kuwa hali ya watu washirikina walio dhulumu katika dunia na akhera ni hiyo tuliyo kusimulia, ewe Nabii, basi usiwe na shaka yoyote juu ya mwisho wa hao katika kaumu yako wanao abudu masanamu pindi wakiendelea katika upotovu wao. Kwani hali yao ni hali ya baba zao walio watangulia, ambao khabari zao tumekusimulia. Wote hao ni washirikina. Na Sisi tutawatimizia kwa ukafiri wao adhabu kaamili kwa kadiri ya makosa yao. Hawatapunguziwa hata chembe.