وَقَالُواْ قُلُوبُنَا فِيٓ أَكِنَّةٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ وَفِيٓ ءَاذَانِنَا وَقۡرٞ وَمِنۢ بَيۡنِنَا وَبَيۡنِكَ حِجَابٞ فَٱعۡمَلۡ إِنَّنَا عَٰمِلُونَ ٥
Waqālū qulūbunā fī akinnatim mimmā tad'ūnā ilayhi wafī ādhāninā waqrun wamim bayninā wabaynika hijābun fa'mal innanā 'āmilūn
Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayo tuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe lipo pazia. Basi wewe tenda, nasi tunatenda. 5
Maelezo ya chini
5 Na makafiri wakamwambia Mtume s.a.w.: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko vizito kwa hayo unayo tuitia yaliyo khusu Tawhidi (Upweke) wa Mwenyezi Mungu. Na masikioni mwetu mna uziwi, basi hayasikii hayo unayo tulingania. Na baina yetu na wewe lipo pazia nene linalo tuzuia kukubali hayo uliyo tuletea. Basi fanya utakalo, na sisi tunafanya tutakalo.