وَلَوۡ جَعَلۡنَٰهُ قُرۡءَانًا أَعۡجَمِيّٗا لَّقَالُواْ لَوۡلَا فُصِّلَتۡ ءَايَٰتُهُۥٓۖ ءَا۬عۡجَمِيّٞ وَعَرَبِيّٞۗ قُلۡ هُوَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ هُدٗى وَشِفَآءٞۚ وَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ فِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَقۡرٞ وَهُوَ عَلَيۡهِمۡ عَمًىۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُنَادَوۡنَ مِن مَّكَانِۭ بَعِيدٖ ٤٤
Walaw ja'alnāhu qur'ānan a'jamiyyal laqālū lawlā fussilat āyātuhū ā'jamiyyun wa'arabiyyun qul huwa lilladhīna āmanū hudan washifā'un walladhīna lā yu'minūna fī ādhānihim waqrun wahuwa 'alayhim 'aman ulā'ika yunādawna mim makāni ba'īd
Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni wangeli sema: Kwanini Aya zake haziku pambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur'ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali. 44
Maelezo ya chini
44 Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni, kama walivyo pendekeza baadhi ya hao wanao kera, basi bila ya shaka wangeli sema: Lau zingeli bainishwa Aya zake kwa ulimi tunao ufahamu! Kitabu hichi cha lugha ya kigeni, na huyu mkhubiri wake ni Mwaarabu! Yawaje haya? Ewe Mtume! Waambie: Hii Qur'ani ni hivyo hivyo kama walivyo teremshiwa Waumini, si wengineo, kuwa ni Uwongofu na Poza kwa Waumini; kiwaokoe na ubabaishi, na kiwaponyeshe na shaka shaka. Na wasio amini wamekuwa kama katika masikio yao pana kizuizi, uziwi, nayo hii Qur'ani kwao wao ni upofu, hawaoni chochote ndani yake ila fitna tu. Hao makafiri ni kama wanao itwa waiamini kwa umbali kabisa. Hawausikii wito huo.