فَإِنِ ٱسۡتَكۡبَرُواْ فَٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُۥ بِٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَهُمۡ لَا يَسۡـَٔمُونَ۩ ٣٨
Fa inistakbarū falladhīna 'inda rabbika yusabbihūna lahū billayli wan-nahāri wahum lā yas'amūn
Na ikiwa watajivuna, basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki. 38
Maelezo ya chini
38 Ikiwa washirikina watajiona wakubwa hawafai kufuata amri yako, basi wewe usiudhike. Kwani hao walio kwa Mola wako Mlezi kwenye utakatifu wake, nao ni Malaika, wanamtakasa Yeye na kila upungufu katika kila wakati, usiku na mchana, wakimsafia ibada Yeye tu, wala hawachoki kumsabihi.