وَمِنۡ ءَايَٰتِهِ ٱلَّيۡلُ وَٱلنَّهَارُ وَٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُۚ لَا تَسۡجُدُواْ لِلشَّمۡسِ وَلَا لِلۡقَمَرِ وَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ ٱلَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ ٣٧
Wamin āyātihil-laylu wan-nahāru wash-shamsu wal-qamaru lā tasjudū lish-shamsi walā lil-qamari wasjudū lillāhil-ladhī khalaqahunna in kuntum iyyāhu ta'budūn
Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu. 37
Maelezo ya chini
37 Na katika dalili za uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni huu usiku na mchana, na jua na mwezi. Msilisujudie jua wala mwezi, kwani hivyo ni katika Ishara zake tu. Bali msujudieni Yeye Mwenyezi Mungu peke yake, aliye umba jua, na mwezi, na usiku, na mchana, ikiwa nyinyi kweli mnamuabudu Yeye peke yake.