Surat Fussilat, aya 35

41:35

وَمَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَمَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٖ ٣٥

Wamā yulaqqāhā illal-ladhīna sabarū wamā yulaqqāhā illā dhū hazzin 'azīm

Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa. 35

Maelezo ya chini

35 Na hawaruzukiwi tabia hii, ya kulipa wema kwa uovu, ila wale wenye khulka ya kusubiri, na hawaruzukiwi hayo ila wenye fungu kubwa la tabia ya wema na ukamilifu wa nafsi.