وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ رَبَّنَآ أَرِنَا ٱلَّذَيۡنِ أَضَلَّانَا مِنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ نَجۡعَلۡهُمَا تَحۡتَ أَقۡدَامِنَا لِيَكُونَا مِنَ ٱلۡأَسۡفَلِينَ ٢٩
Waqālal-ladhīna kafarū rabbanā arinal-ladhayni adallānā minal-jinni wal-insi naj'alhumā tahta aqdāminā liyakūnā minal-asfalīn
Na walio kufuru watasema: Mola wetu Mlezi! Tuonyeshe walio tupoteza miongoni mwa majini na watu ili tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni wa walio chini kabisa. 29
Maelezo ya chini
29 Na makafiri watasema, nao wamo Motoni: Mola wetu Mlezi! Tuonyeshe hayo makundi ya majini na watu walio tupoteza ili tuwaweke chini ya nyayo zetu, wawe katika watu wa chini kabisa.