وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدۡ كُذِّبَتۡ رُسُلٞ مِّن قَبۡلِكَۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ ٤
Wa in yukaddhibūka faqad kuddhibat rusulum min qablika wa ilallāhi turja'ul-umūr
Na wakikukanusha, basi walikwisha kanushwa Mitume kabla yako. Na mambo yote yatarudishwa kwa Mwenyezi Mungu. 4
Maelezo ya chini
4 Na hao makafiri wa kaumu yako wakikukadhabisha kwa uwongofu ulio waletea, basi wewe wastahamilie. Kwani Mitume wa kabla yako walikwisha kadhibishwa vile vile, na wakavumilia kwa walivyo kadhibishwa mpaka wakashinda. Na mambo yote yatarejea kwa Mwenyezi Mungu peke yake.