ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ جَاعِلِ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ رُسُلًا أُوْلِيٓ أَجۡنِحَةٖ مَّثۡنَىٰ وَثُلَٰثَ وَرُبَٰعَۚ يَزِيدُ فِي ٱلۡخَلۡقِ مَا يَشَآءُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ١
Al-hamdu lillāhi fātiris-samāwāti wal-ardi jā'ilil-malā'ikati rusulan ulī ajnihatim mathnā wathulātha warubā'a yazīdu fil-khalqi mā yashā'u innallāha 'alā kulli shay'in qadīr
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliye wafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili-mbili, na tatu- tatu, na nne-nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu. 1
Maelezo ya chini
1 Anaye stahiki sifa njema ni Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye ndiye aliye zifanya mbingu na ardhi zikawa bila ya kuwapo ruwaza ya kuigia mfano wake. Naye ndiye aliye wajaalia Malaika kuwa ni wajumbe kuwatuma kwa viumbe vyake. Wao hao wana mbawa za idadi mbali mbali, mbili-mbili, tatu-tatu, na nne-nne. Yeye huzidisha katika kuumba kwake kama atakavyo kuzidisha. Hashindwi na kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ana uweza mkubwa juu ya kila kitu.